KIPI SIJASIKIA LYRICS BY PROF JAY FT DIAMOND PLANUMZ



niliacha kazi nifanye mzikiwakatabiri nitalost wengine wakanishawishi tuloge
 kuondoa mikosi nakomaa na muziki
 ingawa jua la utosi naamini wote tunapita na kamwe
 jina langu lishatumika sana kutajirisha watu nyota ndogo
walisha sema kuna watu na viatu bunduki
haiuwi watu ila watu ndo wanaua watu
dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu
lisamfire watu wanahusna na wrong fire
tunawaita watakatifu kumbe ndo mavampire

yalisemwa mengi dem wangu alipo toroka
ni fundisho tosha na changamoto kwao
wanachoka nimepitia mengi mitihani ya kila namna
ndo maana mi sishangai wakiniita mbeba lawama
washikaji wengine feki kwenye dili hawakujui
wanazani kila jogoo akiwika ni asubuhi
liziki hamuwezi ziba labda mtaichelewesha tu
mnakesha mnishushe mwenyezi ananipaisha kote
mlikobana kidume ndo nayusua mnanijua
nakamua roho za wanga zinaungua aah

unaehukumu ni wewe
mwenyezi mungu naomba unilinde
 kwenye hii vita milele nami nishike mkono nishinde…

 walishazusha zusha nimekufa
et nimepata ajali washindwe na walegee
mwenyezi niepushie mbali
wakasema nina ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla
wanataka kunizika mzima kabla sijafa
waliosema nina ngoma wengine tushafukia
wanaomba nife leo naamini watatangulia
 mama pumzika pema daima tunakulilia
na bado wanachonga sana
but men the king zia daima
mtaji wangu ni nguvu zangu mwenyewe
 simwamini mtu kamwe najiamini mi mwenyewe
hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe
mi sijali i nope them wote wanalizombe
bado tunapambana kibarua kisiote nyasi
daima sitawadhuru wale wote walioniasi
nikikaa kimya msidhani sijasikia sio
bahati sio kengekewa ni sauti iliyobarikiwa hala!

aah unaehukumu ni wewe
mwenyezi mungu naomba unilinde
kwenye hii vita milele nami nishike mkono nishinde…

No comments:

Post a Comment