HISTORIA YA ALI KIBA

Ali Kiba; Nyota wa muziki aliyerudi kwa kasi katika kiti chake
Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii


Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba, maarufu kama Alikiba.
Baadhi ya watu wamekuwa wakimlinganisha na mwanamuziki nyota kwa sasa Diamond Platnumz, ambaye naye kwa sasa yupo katika nafasi ya juu kimataifa kama ilivyokuwa kwa Alikiba miaka mitatu iliyopita.
Si kwamba ndiyo anaingia katika muziki, kwa watu wanaojua historia ya bongo fleva wanakumbuka kwamba kijana alikuwa tishio, kwani amekuwapo kwenye gemu tangu mwaka 2004 na kufanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha uliojulikana kama ‘Cinderella’.
Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2004, alianza kujituma katika muziki na kufanikiwa kuandika wimbo wake wa kwanza, ‘Maria’. Mwaka huohuo Alikiba alianza kutengeneza albamu yake ya kwanza. Ilipofika mwaka 2005, alipata ofa ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nchini Uganda, lakini baadaye aliachana na mpira ili kuendeleza kipaji chake cha muziki.
Mwaka 2007 alifanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela’, sambamba na kuachia wimbo huo redioni, ambao ulivuma na kusababisha albam hiyo kuuzika zaidi sokoni. Albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2007 Afrika Mashariki.
Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi. Aliifanya Afrika Mashariki kumjua kwa muda mfupi kupitia vibao kadhaa vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu.
2008 Alikiba aliachia albamu ya pili ‘Alikiba 4 Real’ na wimbo wa kwanza kuachia ulikuwa ‘Usiniseme’ na wakati huu alikuwa ameshatangaza jina lake Afrika Mashariki na kwingineko.
Albamu hiyo ilimfanya aanze kuaminika zaidi, mwaka huohuo akateuliwa na kushinda tuzo za Kilimanjaro Music Awards kupitia wimbo wake wa Cinderella.

Aliendelea kutafutwa kwa ajili ya kusakata kabumbu ambapo mwaka 2009, alipokea maombi kwa ajili ya kuichezea timu ya African Lyon ya Tanzania lakini alikataa na kuamua kuingia kwenye mitindo ambako hakukumchukulia muda mwingi.
Akutana na R Kelly
Ilipofika mwaka 2010 ndipo alipopata dili la One 8 na kufanikiwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa akiwamo R Kelly na wengine saba kutoka Afrika. Alipokutana na R Kelly alimsifu kwamba ana sauti nzuri na ya kipekee, hivyo kupendekeza aanze kuimba katika singo ya pamoja ‘Hands Across the World’. Kupitia wimbo huo, mtandao maarufu wa kimuziki duniani Billboard walilitangaza kundi la One 8 kama “Best Bet of 2011” kupitia orodha ya nyimbo zao bora duniani.
Mwaka huohuo Alikiba aliteuliwa na kushinda tuzo ya BEFFTA London Awards kama ‘Best International Artists’ (ACT) na kumshinda mwanamuziki 2 Face Idibia. Pia alifanikiwa kurudi na tuzo ya Sexiest Male Artist.
Historia yake
Alikiba alizaliwa Iringa Novemba 26, 1986 kutoka kwa mama yake Tombwe Njere na Saleh Omari. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wane katika familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba.
Muziki ni kati ya vitu ambavyo zimekuwa vikipendwa na mwanamuziki huyu tangu utoto wake.

No comments:

Post a Comment