MBAGALA LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


Busara na upole
Na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu, Mama
Vyote hukuvijali, huk'ona silingani kabisa kuwa na wewe

Kwa kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu mama
Eti kisa maali, ukaona bora uniache mimi na uolewe
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakua mke wa fulani
N'liumia sanaa, sanaa
Ile siku shekhe namuona anachoma ubani
Unavishwa pete unakua mke wa fulani
Niliumia sanaa, niliumia sanaa, sanaa X2


Tatizo kwetu mbagala, hapa nyumba mbele jalalaaa
Tatizo kwetu mbagala, uk'ona mapenzi siwezi
Ungejua jinsi gani
Machozi n'livyolia kwa uchungu wa penzi langu na
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
Hata kupendwa sitamani
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma
Mwenzio sitamaani, hata raha tena mi sioni
Naskia hivi sasa una mtoto anaitwa mamu
Vile akinuna mpaka tabasamu
M'mefanana sana.a, sana.a
Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu
Tena nna mpango wa kuhama Dar Es Salaam
Nataka niende mba.ali, niepuke vita na walimwengu
Mi mwenzenu siwezi
Repeat x2
 

Mbagala, mbagala, mbagala, mbagala
uk'ona mapenzi siwezi
Mbagala (mbagala), mbagala (mbagala), mbagala (mbagala), mbagala
uk'ona mapenzi siwezi
Repeat x2
I'm back, ladies, I'm back
Bob Junior
Mr. Chocolate Flava
Yo, I'm back, Diamond, I'm back

NIMPENDE NANI LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


chorus
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah


verse 1
kwani nilikuwaga na mpenzi akanizingua,
hivyo nataka muezi kwa haya maradhi naugua
hisije siku miezi na akanisumbua,
ikawa tena kitenzi mzogo kuutua
naogopa sana vijana wa sasa kwenye mapenzi
wasijie wakanitenda,
nikazama na huba mapenzi ya kweli
wakaniacha wakaenda,
we si unajua wazuri ni wengi lakini kumpata mwenye mapenzi ya kweli ndio balaa,
wengi ni wajanja watoto wa mjini wamejawa utapeli tamaa,
wazuri ni wengi lakini kumpata mwenye mapenzi ya kweli ndio balaa,
wengi ni wajanja wa mjini nimpende nani,

chorus
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah

verse 2
yasiwe kama ya wema sepetu kila siku magazeti
ajue nidhamu na mila ya kwetu mjuzi kupeti peti
usimtake ka uwoya ni mtemi ana hasira mpole kama jokate
ila sauti ka wema akiwa analia kicheko kama cha fetty
naogopa sana vijana wa sasa kwenye mapenzi
wasijie wakanitenda,
nikazama na huba mapenzi ya kweli
wakaniacha wakaenda,
we si unajua wazuri ni wengi lakini kumpata mwenye mapenzi ya kweli ndio balaa,
wengi ni wajanja watoto wa mjini wamejawa utapeli tamaa,
wazuri ni wengi lakini kumpata mwenye mapenzi ya kweli ndio balaa,
wengi ni wajanja wa mjini nimpende nani,

chorus
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah
nimpende nani nimpendee eeh
nimpende nani nimpende aah

outro
kwani nilikuwaga na mpenzi akanizingua,
hivyo nataka muezi kwa haya maradhi naugua

KIZAIZAI LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


{Verse 1}
Yanaanza kama safari twende folani ukaone,
Kumbe yana nguvu ni hatari ukishanasa ndio uponie..x2
Mungu aliumba dunia na Maajabu yaake
Ya mwenzako sikia omba yasikupate, eeih ..x2

{Chorus} x2
Nyie Mapenzi yanauma (Kizaizai)
Yanaumiza (Kizaizai)
Oooh kizunguzungu jamaa mapenzi mabaya
Weza gombana na Ndugu (Kizaizai)
Rafiki akawa Mubaya (Kizaizai)
Kazi ukaona chungu (Kizaizai)
Nyie Mapenzi karaha (Kizaizai)

{Verse 2}
Yananyima furaha....
Yanakosesha raha....x2
mmmmm
Tena usiombe kupenda uliempenda ajuee
Tena usiombe kupenda uliempenda ajue
Amani utakosa Karaha jamani eeeh..
Dunia tena chungu kufa utatamani eeh..
Mungu aliumba dunia na Maajabu yake
Ya mwenzako sikia omba yasikupate, eeih ..x2

{Chorus}
Nyie Mapenzi yanauma (Kizaizai)
Yanaumiza (Kizaizai)
Oooh kizunguzungu jamaa mapenzi mabaya
Weza gombana na Ndugu (Kizaizai)
Rafiki akawa Mubaya (Kizaizai)
Kazi ukaona chungu (Kizaizai)
Nyie Mapenzi karaha (Kizaiza
Baba na mama watake
Chakula tamu ni sumu
Mashoga sasa wanafiki
Kulala nanyi ni ngumu
eeh yanauma tena yanauma

KESHO LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


{Chorus}
Mi nataka kesho twende nikupeleke nyumbani
nataka kesho twende ukamuone mama x2

{Verse 1}
Kwanza kabisa ntanyonga Tai
T"shirt na Jeans ntatupa kidogo..
Unite Nasibu usiniite Dai
Asije kukuona muhuni akapandisha Mbogo...
Naukifika uagize Chai
Savanna Takila uzipe kisogo...
Kuhusu mavazi kimini haifai
Tupia pendeza ila za Hekima Logo...
Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2

{Chorus}
Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

{Verse 2}
Usilete swaga za Nainai
Ukanyoa kiduku kama Moze Iyobo..
Eti shoping twende Tai
wakati Dadaangu anaduka kigogo..
Ukikuta Nguna usikatae
we zuga unapenda hata kama wa Muhogo..
Kuhusu kabila mbona Sadai
Mama angu hana noma hata kama Mgogo
Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2

{Chorus}
Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

Mama yangu mama...
Mama Naseeb mama...
Mama Diamond mama...
Mama yangu nyumbani...
Mama Chali mama...
Mama Sepetu mama...
Mama Kidoti mama...
Kwa mama Diamond nyumbani...

MAWAZO LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


(Chorus)
Ningekuwa na uwezo ningekunywa hata pombe ili nipunguze mawazo,
maana mchana kutwa hata usiku silali mapenzi kwangu kikwazo.

(VERSE 1)
Sikujua mapenzi balaa tena ni maladhi ya moyo kupendaga...
tena mapenzi karaha yanajenga chuki na choyo kwenye kava...
Utu wangu unathamani inamaana kweli hakuvijua!
Licha ya burudani namapenzi yangu akayatimua,
Utu wangu unathamani inamaana kweli havijuaa!
Mmmh! Licha ya burudani ndani akaamua kutimuaah! (Inauma sana)

(Chorus)
Ningekuwa na uwezo ningekunywa hata pombe ili nipunguze mawazo,
maana mchana kutwa hata usiku silali mapenzi kwangu kikwazo X2

VERSE2
Ona jini kisirani kaingia kwenye utamu wa penzi langu
ameleta tafarani naumia nalia na moyo wangu...
Ona jini kisirani kaingia kwenye utamu wa penzi langu,
ameleta tafarani mwenzenu nalia na moyo wangu.
Kweli wivu me ninao na roho yangu inaumiaa,
kweli wapenda nao ndo maadui zikitimia!
Lile tunda langu la mara leo limekuwa sumu kwangu,
ona tena sina raha me nacheka nalia na moyo wangu.

(Chorus)
Ningekuwa na uwezo ningekunywa hata pombe ili nipunguze mawazo,
maana mchana kutwa hata usiku silali mapenzi kwangu kikwazo X2

MOYO WANGU LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


(Chorous)
Moyo wangu..Moyo wangu mama..
Moyo wangu mimi umeniponza mama!
Moyo wangu,Moyo wangu mama,
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

(Verse one)
Upole wangu simanzi Eeeh!
Kwangu kupenda maradhi iiih!
Lakini kupendwaga mi nae bahati huwaga sina...
jichoni kwangu kibanzi Eeeeh!
ninakapenda kamanzi Iiih!
Oooh Licha ya kumthamini kama shilingi tatizo hata raha sina....
Ufinyu wa mboni zangu, unatazama mengi yanayonipa mateso,
Ukweli hatakupenda sina raha! ona nakonda kwa mawazo.
Masikini penzi langu jina lishakatwa na kauli roho inatoka kesho
Kutwa nzima mara Eeeh! Mara Iiiiii! Hata najuta kupenda....

(Chorus)
Moyo wangu..Moyo wangu mama..
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa!
Moyo wangu,Moyo wangu mama,
Moyo wangu mimi umeniponza mamaa

(Verse two)
Nikutwa kucha maneno,kosa si kosa maneno ilimradi tu karaha tantalila!
(Sina raha)
Ona sina tena mipango (aah ho aah!)
Kutwa nzima nnamawazo jina Mh!
aaaah! Sina raha Oooh! mama
Tamu ya wali ni nazi Eeeh!
Raha ya supu mandazi iiih!
Raha yangu me kupendwa tu naye lakini nyota sina.
Laana napata na radhi Eeeh! Nawakufuru wazazi iii!
Kwakung`ang`ana me kutaka kuwa nae lakini bahati sina!
Masikini roho yangu (roho yanguu) ingelikuwa ni nguo ningempa avae
Kkila kona akipita wamsifie ila lakini ni kikwazo
Masikini penzi langu jina lishakatwa na kauli roho inatoka kesho
Kutwa nzima mara Eeeh! Mara Iiiiii! Hata najuta kupenda

UKIMWONA LYRICS BY DIAMOND PLATNUMZ


mmmmhhhh
Mungu aliumba dunia mapenzi tangu na tangu
yashanipiga sasa sinabudi nielewe
siwezi kung'ang'ania huenda sio fungu langu
japo nishida ila, nitabaki mwenyewe
ohh ila , mpe shukrani kwa kuniumiza suraya
mwambie mi bado mahututi nauguza kidonda changu
na asisikie kisirani, hukumu ya mapenzi mabaya
hata ungali hai kayruki usingetibu gonjwa langu
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyooo)
sina amani nasaka rumba (oohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona

ukimuona ukimuona
ukimuona ukimuona ukimuona
we nenda mwambie marafiki, marafiki wabaya
tena wengi waongo, hawawazi ndanganye
oya ni mashoga rafiki, oohh marafiki wabaya
oooohhhh oooohhh mmmmmhhh
tatizo mi bado, nilipoteleza nkakosa sipajui
mpaka akafunga virago, na akaamua kuondoka sitambui
ubaya, kinacho niumiza, maneno neno maneno
mara kwa ndugu rafiki, kwanini anawapa misemo
najaribu papasa, mbona ka macho ataona chochote
ila ndo kutwa mikasa, na nazidi kuanguka, niokote
kutwa nzima moyo unanidunda dunda (dunda)
sina amani nasaga rumba (rumba)
ohh unani dunda
sema chine tembee moyoo
unanidunda dunda (mamii moyoo)
sina amani nasaga rumba (ooohh mimii)
ohh unani dunda
eeeeeeehhhhhhhhhh ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona, ukimuona
ukimuona