DOWNLOAD OUR ANDROID APP HERE
[Verse 1]
Nataka nitoke
kwenye gazeti
Niuze sura!
Niseme ninatoka na
Jokate...
Kitandani kwisha na
Feza Kessy
Ama Snura
Nilete matata mpaka
kwa Grace
Kwenye redio zote,
mpaka runinga
Nitangaze kwa
kuvimba
Kwamba Lulu ana
yangu mimba
Au niwatukane wote
wanaoimba
Kwa dharau na
kuvimba
Mpaka yule anajiita
Simba!
Niseme madam Ritha
katetema
Akiniona anashindwa
hata kuhema
Au Vanessa kanena
ananitaka na Jux atatemwa
Nataka nifanye
sinema
Kwa alozaa na Ney,
Siwema
Kiki ipi iko njema,
au niende kwa Sepetu Wema?
[Chorus]
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
[Verse 2]
aaaaa aaaa eeee
Nasikia Uwoya
mkali, wanasemaga Shishi asali
Wolper atakubali
akimwage ki Harmo chali
Ninatafakari,
kichwani maswali
Nimtongoze Zari,
akijua Mondi si hatari?
Ee-hee, Rose
Ndauka, Kajala pia hadi na Salama
Mose Iyobo
asijeninua kwa Aunty lawama
Mkubwa Fella, Tale
Salami leaders nizushe pesa wamenipiga
Chege na Madee
wasije nikwida
Iyowee!
Nataka nibadili
ratiba, kwangu isije leta msiba
Nitoke Wasafi
niende kwa Kiba
[Chorus]
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
Ati ntokeje?
Mwenzenu ntokeje?
[Outro]
Nataka nifanye
masekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Yaani Bongo nzima
makelele
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Iih! Nikinukishe
kinoma noma
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Sekere
(Sekere oh sekere)
Iih! Macho kuvimba
wataisoma
(Sekere oh sekere)
(Sekere oh sekere)
(Sekere oh sekere)
Ta ntira rara
My favorite song... My favorite artist
ReplyDelete