GUNDU LYRICS BY LAVA LAVA


[Verse 1]
Naona Maajabu,
Kinanizonga Kizaazaa.
Kila Mahesabu,
Ninayopiga Yanakataa.
Nahisi Mababu,
Mizimu Yao Imechachamaa.
Au Sina Thawabu,
Mola Nionyeshe Nyota Ya Jaa.

Kulia Nimelia
Nikamaliza Leso
Nimekosa Kipenda Roho.
Mi Nikasubiria
Huwenda Akaja Kesho
Nilipodososa Kote Ngoma Droo. [Chorus]
Mwenye Mapenzi Atokee (Anitetee)
Joto Pepeee (Anipepee)
Niwe Mtoto Tete (Oh Tetee)
Anidekee (Dekeedekee)

Eeeeh
Niepuke Gundu (Oooh Gundu)
Penzi Linanichachia Gundu (Oooh Gundu)
Nuksi Imenishukia Gundu (Oooh Gundu)
Penzii Chachiaa Gundu (Oooh Gundu)
Nuksi Imenishukia Gundu. [Verse 2]
Ama Sina Bahati
Jini Gani Kanivaa
Asio Na Jema Kwangu.
Ninaemtaka Simpati
Vioja Tu Na Karaha
Yani Vanguvanguu.
Nahisi Nalala Na Bundi
Najisonyasonya.
Penzi Sasa Bila Hudi
Ni Malonyalonya.
Nishapangwa kwa Makundi
Nikabonywabonywa.
Licha Ya Wangu Ufundi
Nikapokonywa. [Chorus]
Mwenye Mapenzi Atokee (Anitetee)
Joto Pepeee (Anipepee)
Niwe Mtoto Tete (Oh Tetee)
Anidekee (Dekeedekee)

Eeeeh
Niepuke Gundu (Oooh Gundu)
Penzi Linanichachia Gundu (Oooh Gundu)
Nuksi Imenishukia Gundu (Oooh Gundu)
Penzii Chachiaa Gundu (Oooh Gundu)
Nuksi Imenishukia Gundu.

No comments:

Post a Comment