Verse 1
Kama mama anavyompenda mwana toka tumboni,
Nami ndivyo nilikupenda tangu zamani,
Moyo uliniuma pale ulipo weka donda
Nafsi ilisononeka huku ikisema,
Moyo uliniuma pale uliponiogopea,
Nafsi ilisononeka huku ikisema,
Kamwe sitopenda maishani na dunia,
Wewe ubaki pekeako na mimi kivyangu,
(chorus)
Nia yangu nisikuwaze ,
kwenye moyo wangu unitoke,
ili moyo upoe, na donda la moyo lipone,
Nia yangu si mbaya ,
Najinusuru mapema,
Akijikwaa mmoja na me wa nyuma kujikinga,
Verse 2
Ulipokuja kuishi na me kama mwandani,
Mwenyewe si ulitabiri uzuri wa sura na busara pia
(Kwa kupenda nilijisumbua,
Kupenda hasiye pendeka,
Moyo wangu naomba uachie upumue,x2)
(chorus)
Verse 3
Nia yako unilize
Moyo wangu utese *delee
Kosa lako unanigeuzia mie,x2
Nimekushtukia ,unaiogopea wewe,
Kosa lako unanigeuzia mie,x2
(chorus)
No comments:
Post a Comment